TAPO Logo

TAPO Logo

Wednesday, July 12, 2006

Hali Bora kwa Wanyama

HALI BORA KWA WANYAMA


Hali bora kwa Wanyama wanaotumiwa na Binadamu inatokana na jinsi ya kukubaliana na mfumo wa maisha bila ya kuteseka kwenye mazingira yaliyotayarishwa na binadamu.

Wanasayansi na Wanafilosofia wanatambua kuwa Wanyama wana akili ya kuendeshea maisha yao na hata hali ya mwili {afya na utambuzi wa mwili} ambavyo vinaweza kudhuliwa kwa jinsi gani Binadamu wanavyowatendea na kuwahifadhi.

Aina Tano za uhuru zinatumika kuelezea mahitaji yote ya Wanyama wa kufugwa na wajibu wa kuwatunza kama ifuatavyo;
Uhuru wa kutokuwa na maumivu, majeraha na magonjwa.
Uhuru wa kutokuwa na njaa, kiu, na utapiamlo.
Uhuru wa kuonyesha tabia ya kawaida.
Uhuru wa kutokutishwa na kutokusumbuliwa.
Uhuru wa kutokukosa raha ya mwili

Aina Tano za uhuru zinaweza kufikiwa kwa mfano,
Kuwatayari kuwapatia uwezekano wa maji safi ya kunywa, chakula bora cha kujenga afya ya mwili,na katika hali ambayo wanyma wamepewa chakula kwa kipimo, kufanya uwezekano wa kupatikana aina nyingine ya chakula kama vile majani ili kumridhisha mnyama
Kumpatia mazingira bora ambayo ni pamoja na kimvuli, nyumba ya kuishi, na sehemu nzuri ya kupumzikia.
Kuzuia na katambua haraka na kutibu magonjwa na majeraha, kumpatia chanjo pale inapobidi, kudhibiti mzunguko wa sehemu bora ya malisho ili kupunguza maambukizi ya magonjwa,
Mnyama apatiwe nusu kaputi haraka pale ambapo matibabu yataleta maumivu ya muda mrefu {kwa mfano kuvnjika kwa miguu}. Usimsafirishe mnyama mwenye majeraha au ugonjwa,au mnyama aliyefikia hatua za mwisho za ujauzito, labda iwe unampeleka kwa mganga wa mifugo au kwenye matibabu yenye faida kwa mnyama{kwamba usimsafirishe mnyama wa aina hiyo kwenye machinjio au sehemu myingine ambayo mwisho wake ni kuchinjwa }



No comments: