Mradi wa Kuwasaidia Punda
“Hali Bora na Afya Bora”
Msimazi wa Mradi; Yohana Js Kashililah
Walengwa; Wakazi wa Wilaya ya Kahama na Punda wao
Tarehe ya kuanzia; September, 2006
1. Maelezo ya Mradi
Shirika la Hiari la Kutetea Haki za Wanyama Lijulikanalo kwa jina la TAPO yaani Tanzania Animals Protection Organization, litabeba jukumu la mradi wa kuwasidia punda katika wilaya ya kahama.
Wilaya ipo umbali wa kilomita zipatazo 221 kutoka Shinyanga Mjini katika Tanzania Bara iliyo ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Walengwa ni wakazi wa wilaya ya kahama pamoja na punda wao katika kata zote 34 yenye ongezeko la watu wapatao 679.829, asilimia kubwa ya wakaazi wote wanamiliki punda, na ndio watakaohusiswa katka kuhamisishwa kujali hali bora na afya bora za punda wao katika kata zao.
Kuna idadi ya punda wanaokadiliwa kufikia 3428 katika wilaya yote ya kahama {kutokana na ripoti ya idadi ya mifugo wilayani kahama 2001}, isiyokuwa na huduma za kituo cha afya ya mifugo. Asilimia kubwa ya wakazi wote wanajishughulisha na kilimo, na asilimia kubwa ya wakulima wanamiliki au wanamtumia mnyama aitwaye punda na wanyama wengine katika shughuli zao za kila siku, na kuna kati ya punda mmoja mpaka wanne kwa familia moja.
Punda wanatambulika kama watendaji,watoa huduma, na wanaofaa katika kusaidia ukuaji wa uchumi kwa ajili ya kukabiliana na mkakati wa kupunguza umaskini miongoni mwa jamii ya watu wa kahama, kwa ufupi punda ni muhimu katika usafiri na kazi za kilimo.
Mkokoteni wenye kuwa na mti mkubwa mmoja na punda wawili waliofungwa kwenye shingo, punda wanabeba uzito kwa kuvuta mkokoteni kupitia kwenye shingo zao nyembamba zilivofungwa kamba.
Uzito wote wa kuvuta mkokoteni unategemea shingo ya punda ambayo kutokana na uvutaji huo punda hupata maumivu makubwa na majeraha makubwa, kamba mara kwa mara zinaingilia uwezo wa kupumua.
Na hii ndiyo sababu kubwa inayowanyima raha punda na kuwaletea vidonda vikubwa.
Uwezo wa ubebaji wa punda kahama ni wa kuzidi na kuwatisha kuliko uwezo wa punda wa ubebaji wa kawaida.
Wanabeba mizigo kupita kiasi, kubeba asilimia 100 zaidi ya uzito wa mwili wao kwa umbali mrefu, uzito wote kuwa sehemu moja bila ya kuwa ya kuwa na aina ya Kilinganisho, ambapo baadhi ya watu wanambebesha punda mizigo kwa upande mmoja kwa kutumia kamba au kitu kingine chochote, hii inaweka mgandamizo mkubwa katika uti wa mgongo, mara kwa mara wanaanguka njiani, kwa muda mrefu wanakuwa na njaa na kiu.
Punda wengi wanafugwa kwa ajili ya usafiri, kama ni kwa ajili ya kubeba au kuvuta mkokoteni- kupitia madhumuni ya kusafirisha mazao ya mashambani, kuni, maji, mbolea, kukodisha, vifaa vya ujenzi kama vile mchanga, mawe, kokoto, saruji na shughuli nyingine
Usafirishaji wa mazao na shughuli zote za kilimo ndio unaongoza kwa wakulima kutumia punda wakati wa msimu wa kupanda na kuvuna kata nyingi wilayani kahama, ambapo mashamba yapo umbali wa kilomita kadhaa kutoka katika makazi ya wakulima, inachukua kiasi cha masaa manane kwa siku, na hata wakati wa usiku utakuta punda bado wapo kazini, wakipita kwenye njia yenye mawe, kwenye mabonde na milima.
Utengenezaji mbaya wa mkokoteni na ufungaji kwa punda ni tatizo kubwa linalosababisha majereha mengi kwa punda wa kahama, ambapo punda wanavuta mkokoteni kwa kutumia shingo badala ya kifua.
Hali za punda wengi ni wa kahama ni dhaifu kuanzia muonekano wa mwili mpaka mpangilio wa kiafya, wengi wana majeraha kwenye shingo,kifua,mkiani,katika miguu,usoni, kwato zina majeraha na zimeongezeka zaidi
Wamiliki wa punda wanawathamini punda wao kwa ajili ya kufanya kazi tu siyo kuwathamini katika hali bora na afya bora, hivyo mradi huu unalengo la kutoa elimu kwa wamiliki wa punda wilayani kahama kuhusiana na kuwahamasisha kuwapatia hali bora na afya bora punda wao kwa kutumia mbinu zifuatavyo;
2. Elimu na Mazoezi ya kazi
Kutakuwa na maelezo kamili katika mafunzo ya wamiliki au mtumiaji wa punda katika kutambua hali bora kwa punda, hali bora ya afya ya punda, kumzoesha punda mazoezi ya kufanya kazi, ambapo wamilki au watumiaji watawafanyisha mazoezi punda katika hali ya kutambua ni wakati gani punda wanakataa kufanya kazi zaidi.
Mafundisho mazuri yana faida kwa shughuli yote ya ufanyaji kazi iwapo itajumuisha udhibiti na utoaji amri kwa punda,na kwa kutakuwa na siku za mafunzo ya darasani kwa kila kata kama ifuatavyo
1. Elimu Kuhisiana na Malazi ya punda
Elimu hii itajumuisha kumpatia punda malazi bora yanayofaa kwa misimu yote ya hali hewa ya mwaka, kutokana na kuwa ngozi haina uwezo wa kuzuia maji- hivyo malazi bora ya punda yatamlinda katika baridi kali, na kumpatia kimvuli katika siku za joto, na kuepukana na wadudu warukao kama n’zi.
2. Elimu kuhusiana na Malisho ya Punda
Elimu hii itajumuisha wamilki au wahudumu wa punda kutambua njia gani za kumpatia malisho bora, kumlinda na majani yenye sumu na kumlinda na ugonjwa utokanao na kula kupita kiasi
3. Elimu kuhusiana na afya ya msingi ya punda
Elimu hii itajumuisha wamiliki au wahudumu wa punda kuchunguza punda kama wanaugua au wanauwezo wa kufanya kazi kwa wakati huo, au kutambua kitu chochote tofauti katika afya ya punda kabla ya kumwita mganga wa mifugo.
Kumfanyisha kazi punda asubuhi sana na jioni, kupumzisha kila mara katika kivuli na muda wa kumpatia maji, kupunguza kwato zilizoongezeka.
4. Elimu Kuhusiana na Kumtendea punda
Elimu hii itajumuisha kumtendea punda katika kuvuta mkokoteni, na ubebaji wa mizigo, jinsi gani ya kupunguza maumivu na majeraha yatokanayo shughuli nzima ya uvutaji mkokoteni kwa kuelimisha kuhusiana na utengenezaji mkokoteni usio kuwa na madhara kwa punda
3. Malengo ya Mradi
Mradi wa kuwasaidia punda wa kahama una dhamana ya kuhamasisha na kulinda afya, usalama na hali bora ya punda wote wapatikanao wilayani Kahama Mkoani Shinyanga. Miezi sita ya mradi huu itasaidia kuwasogeza wakaazi wa kahama kuwaelewa na kuwaheshimu Punda wao kama viumbe hai kwa malengo yafuatayo;
· Kubuni, kukabiliana na kuhamasisha jambo lolote linalohusiana na punda katika kuwapatia hali bora na afya bora kupitia kwa binadamu.
· Kuelewesha, kukubalika, kufufua na kuendeleza hali bora na afya bora za punda katika jamii wa watu wa kahama.
4. Umuhimu wa Mradi Huu
Ni lazima kufanya mradi huu kwa wakati uliopangwa kutokana na unyanyapaaji na unyanyasaji wa punda katika jamii ya watu wa kahama ni wa hali ya juu sana
5. Usimamizi wa Mradi
Mradi wa kusaidia punda wilayani kahama utasimamiwa kwa karibu kabisa pamoja na ushauri kutoka Kitivo cha Elimu ya Magonjwa ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine {SUA}, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo, Halamashauri ya Wilaya ya Kahama, Mganga wa Mifugo Wilaya ya Kahama, Maofisa Watendaji wa Kata, Mashirika ya Hiari, Vyombo vya Habari na Jamii kwa ujumla ili kuleta Hali Bora na Afya Bora na kutekeleza na kufanikisha malengo kamili ya mradi.
Mfumo wa usimamizi wa mradi ni;
1. Kundi la Usimamizi wa Mradi
Kundi hili linatokana na Wanachama na Wafanyakazi wa TAPO,Madaktari wa Mifugo waliofuzu na kusajiliwa, wataendeleza usimamizi wa kila siku wa shughuli za mradi, kwa kufuata ratiba ya kazi, mpangilio wa bajeti, kuhakikisha kuwa kuna mawasiliano ya kutosha pamoja na washiriki wengine wa mradi na vikundi vingine vya hiari.
2. Kundi la Ushauri la Mradi
Kundi hili linatokana na Wafadhili mbalimbali wa mradi, Wahadhili kutoka Kitivo cha Elimu ya Magonjwa ya Wanyama-Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Morogoro {SUA}, Madaktri wa Magonjwa ya Wanyama kutoka Wizara ya Maendeleo ya mifugo, na Madaktari wa mifugo kutoka kata zote 34 za wilaya ya kahama.
Kazi za Mradi
Mradi huu unategemewa kuchukua miezi sita {6} kwa kupitia.
Kuchunguza hali iliyokuwepo
Uchunguzi kamili wa hali iliyokuwepo, afya ya punda na hali ya kuwatendea vitafanywa kupitia madaktari wa mifugo waliofuzu na kusajiliwa kwa kudadisi kuhusu
.
Matumizi ya punda
· Aina ya mizigo
· Dhumuni la kubeba
· Matumizi ya mara kwa mara
· Jinsi ya kubeba
· Uwezo wa kubeba
· Njia watumiayo kupita
Malisho
· Chakula
· Maji
· Mengineyo
Ukaguzi wa afya ya wa nje
· Masikio
· Ngozi
· Miguu
Kuendeleza Malengo na Madhumuni
Washiriki wataendeleza mikakati ya kuendeleza malengo ya mradi na madhumuni kwa kufanikisha mikakati kwa kushirikiana na Asasai za Serikali, Mashirika ya Hiari na watu wengine wote kwa kuzunguka Wilayani kahama na kutoa matangazo ya kuhamasisha vipeperushi.
No comments:
Post a Comment