Upendo Kwa Punda
Punda ni Mnyama Mstaarabu, Mtulivu na mwenye akili, na ni kiungo muhimu sana kaika kusaidia shughuli nyingi za maisha ya baadhi ya binadamu.
Punda ni mnyama rafiki sana kwa binadamu kwani anatabia ya kukubali kufuata matakwa ya binadamu. Kwa ujumla ni mnyama mwenye upendo wa hali ya juu sana
Punda anapatikana sehemu nyingi ndani ya nchi yetu ya Tanzania, na watu wengi sana wanawatumia punda katika shughuli za Kilimo, Ujenzi na hata Usafirishaji.
Pia ikumbukwe kuwa Bindamu ni mnyama, ana hisia za maumivu, ndivyo hivyohivyo kwa punda kuhisi maumivu
Kuwa na punda halafu humpatii chakula cha kutosha, kumtibu na kumuangalia afya yake ipasavyo, kumbebesha na kumvutisha mizigo yenye uzito mkubwa ni Ukatili wa hali ya juu sana, na ni uvunjaji wa sheria za haki za wanyama Tanzania.
Kitendo cha kuona punda wako ana vidonda shigoni au sehemu nyingine yeyote ya mwili na, bado unamtumia kufanya shughuli yako kupitia vidonda vyake ni Utesaji na Ukatili wa hali ya juu sana.
Ushauri wa Huruma
Muhudumie punda wako kwa huruma, upendo na heshima kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi
Punda kwa ajili ya kuvuta au kubeba mizigo ni lazima wawe na umri kati ya miaka 4 na 25
Punda kwa ajili ya kubeba na mwenye uzito wa kilo 160 ni lazima asibebe zaidi ya kilo 50.
Punda wa kuvuta asivute kupitia shingoni, avute kupitia kifuani na mpunguzie maumivu kwa kumvalisha sponji nene au kitu kingine chochote laini
Punda wa kubeba mpunguzie maumivu kwa kumuwekea sponji, canvass au kitu kingine chochote laini.
Mchunguze punda wako kila siku kuona kama ana matatizo ya kiafya kwa kumpeleka au kumwita mganga wa mifugo.
S.L.P 62921 Dar es Salaam,
No comments:
Post a Comment