TAPO Logo

TAPO Logo

Tuesday, July 18, 2006

TWIGA

TWIGA


Twiga: Giraffe: Giraffe Camelopardalis
Wanapatikana: Africa, Kusini mwa jangwa la Sahara, kwenye miti ya
Wazi Na kwenye majani.
Urefu mpaka mapembe: Dume, mita 4.7-5.3, jike mita 3.94-5
Uzito: Dume, kilo 800- 1930, jike, kilo 550-1180
Tabia: Wanajitenga kimakundi
Umri wa kuishi: Miaka 25 wakiwa porini
Chakula chao: Majani kutoka juu ya miti, majani ya kwenye vichaka,
Mizizi nk.
Sauti: Kawaida huwa kimya, lakini wanapiga chafya, mtoto hulia
Kama atachanganyikiwa.

Kuna subspecies tisa za twiga zinazotambulika, zote zinafanana lakini zinatofautiana kwa michirizi ya rangi, na mgawanyiko wa kijiografia.
Twiga ni viumbe wastaarabu, lakini hawajiweki kwenye makundi, badala yake wanakutana kimakundi kila siku, lakini mchanganyiko wa kundi unatofautiana kila siku baada siku. Twiga dume wa sehemu Fulani huwa anaanzisha hali ya kusachi kwa kurefusha shingo.Iwapo dume mgeni ataingia makazi ya dume mwingine atafukuzwa na dume lenye makazi yake, na wote wawili watagombana kwa kugonganisha vichwa vyao mpaka mmoja wao atakaposhindwa. Fuvu la dume twiga ni gumu zaidi kwa sababu hiyo.

Uzaaji: kubalehe Kwa twiga jike Ni kati ya miezi 48-60, twiga dume Ni miezi 42. Twiga wanapandana wakati wowote Kwa mwaka Na mimba kubebwa kati ya siku 450-464. Huwa kunakuwa Na mtoto mmoja anayezaliwa, mapacha ni adimu kuzaliwa.
Twiga jike katika msimu huwatamanisha madume yaliyo karibu naye, lakini Ni dume mkumbwa tu ndiye anayeshinda. Dume lililoshinda huwafukuza madume wadogo Kwa kuwatisha: kupigana, siyo lazima katika hali hii. Mimba ya twiga huishia miezi 15 baada ya hapo huzaa Na mama Na mtoto wa twiga watakwenda sehemu au uwanja wa ushirikiano unaotumiwa Na majike muda kwa muda na mtoto wake tu hapo. Watoto wa twiga wanazaliwa Na mapembe, ambayo siyo kawaida. Mapembe yanalala kwenye fuvu la mtoto wakati wa kuzaliwa, lakini yatajinyoosha mara baada ya wiki kwanza kuzaliwa .
Uwanja wa kutunzia watoto huwa kuna kuwa na mtoto mdogo wa twiga kila mara ataachwa na watoto wenzie wenye kufikia umri sawa wakati mama yake atakapo kwenda kutafuta chakula wakati katikati ya siku. Hata hivyo watoto wa twiga wanawindwa Sana na fisi, chui na mbwa mwitu, na ni nusu yao ndio tu watakao pona katika muda wa miezi sita ya kwanza.
Jinsi mtoto anavyokuwa mkubwa atajiunga na mama kwenda kutafuta chakula. Simba ndio adui Yao mkubwa, lakini twiga anauwezo wa kumuua simba iwapo Kama atamsukuma kwa nguvu kwa kutumia miguu yake ya mbele. Baada ya watoto wa twiga kufikisha umri wa mwaka mmoja ni wachache kati ya mmoja kwa kumi atakufa kwa mwaka.
Kujitegemea kwa twiga kunachukua miezi 15 ingawa mama yake atakutana tena na dume miezi 5 baada ya mtoto kuzaliwa, twiga kijana wa kike anakaa na mama yake, lakini twiga kijana wa kiume atakwenda kujiunga na umoja wa madume wote na kwenda kutembea peke yake atakapofikisha umri kiasi cha miaka 3.

Chakula: Twiga ni wanyama wanaokula majani na hula majani miti na vichaka. Wanatofautiana katika ukusanyaji wa chakula na kutegemea na nini anacho kula.
Baadhi ya miti Kama vile acacia, ina miba mingi Sana, hivyo twiga anahitaji kuwa makini wakati atakapokuwa ana kula chakula kutoka kwenye miti hiyo. Huwa wanamega majani na mikungu ya majani na kuwacha miiba pekee Yao. Ulimi wa twiga unaweza kufikia sm 45 kwa urefu, na hutumia kusukuma majani ndani ya mdomo na kupaka chakula chote kwa mate yanayovutika kufanya chakula kiwe rahisi kumeza.
Jinsi twiga wanavyotumia kutafuta na kukifikia chakula inapunguza ushindani katika jinsia. Twiga jike ana inama chini ili kufikia matawi ya majani ya chini na vichaka, lakini twiga dume anarefusha shingo yake kufikia majani ya juu ya miti. Twiga jike anakula mpaka kufikia masaa 12 katika kila masaa 24, lakini dume linakula muda mchache. Dume linakula kiasi cha kilo 60 za majani Kwa siku.

Uhifadhi wa twiga
Twiga ni mnyama aliye ma mvuto katika kumwangalia na hata jinsi anavyotembea kwa mwendo wa madaha kutokana na urefu wake ambapo kuanzaia kichwa, shingo, mwili na hata mguu inavyotingishika
Ili twiga na vizazi vyake vijavyo waweze kuishi pasipo bughudha ya binadamu popote pale ndani ya nchi ya Tanzania na majirani zake, tunahitaji kuwa na huruma na upendo na kuheshimu viumbe hawa kwa kuwasaidia kwa hali yeyote watakapo patwa na jambo lolote la kutishia uhai wao, ikiwa pamoja na kuzuia ujangili na uwindaji, utumiaji wa bidhaa zitokanazo na twiga, kuhifadhi na kulinda mazingira ya wanyama hawa wanayoishi, kama vile kutokuchoma moto mapori, kutupa kitu chochote kile kitakachowadhuru mwili na uhai wao kwa ujumla, na kuwalinda kutopata magonjwa.