TAPO Logo

TAPO Logo

Friday, July 21, 2006

Kunguru

KUNGURU
Kunguru wa Zanzibar


Jina la kisayansi anajulikana Kama “corvus splendens”

Historia yake katika Tanzania:

Kunguru hawa Kwa mara ya kwanza walipelekwa katika visiwa vya Zanzibar kutoka katika mji wa Bombay na serikali ya India mwaka 1891 mara baada ya kuombwa na Sir Gerald portal. Waliletwa kunguru 50 Kwa ajili ya kudhibiti uchafu na takataka zinazoweza kuliwa na ndege hawa katika sehemu ijulikanayo kama “Stone Town.”
Ulipofika mwaka 1917 uzalianaji wa kunguru uliongezeka sana na kufanya waonekane kama ndege waharibifu sehemu ya stone town. Kunguru Siyo tu wanadhibiti takataka zinazooza tu, Bali pia wanakula wanyama wadogowadogo (Kama panya), mazao ya mbegu, matunda na mazao mengine.

Lakini pia kunguru wanashindana na aina nyingi za viumbe tofauti kwa chakula. na katika sehemu za viota vya ndege moja kwa moja wanakula vifaranga na mayai kutoka kwa ndege wengine. Huu ni ukweli kuwa sehemu ambayo wanapatikana kunguru, ndege wametengeneza viota sehemu ambayo kunguru hatofikia, na siyo rahisi kukuta ndege amejenga kiota kwenye mti, tofauti na sehemu ambayo hakuna kunguru utakuta ndege wamejenga kiota kwenye miti na sehemu nyingine ya wazi kabisa.

Utambuzi

Kuna aina sita (6) ya kunguru duniani, na kunguru ni huyu wa Zanzibar ndiye kunguru mdogo kuliko wengine katika jamii Yao [sm 43]. Ana rangi nyeusi ikitapakaa sehemu kubwa ya mwili na rangi ya majivu kwenye shingo na kifuani, wana macho ya kahawia wakiwa wakubwa.
Vifaranga vya kunguru vinafafana na kunguru wakubwa, lakini wana macho meusi na mdomo wa ndani huwa unakuwa na rangi ya pink.

Chakula chao

Kunguru wana aina nyingi ya chakula,
Chakula chao ni pamoja na:
Mbegu- karanga, mahindi nk
Matunda
Wadudu
Wanyama wadogo wadogo
Mayai
Mizoga, nk.

Uzaaji wao.

Kunguru ni jamii ya ndege, na hutengeneza kiota kikubwa kilicho na umbile kama la bakuli, kwa kutumia vijiti, majani, magome ya miti na manyoya. Kiota hujegwa kwa ushirikiano wa kunguru dume na jike, mayai hulaliwa na jike tu, na kifaranga mmoja huzaliwa kwa mwaka, kifaranga hulishwa na dume na jike

Kusambaa Kwa kunguru.

Kutokana na jinsi kunguru wanavyozaliana kwa wingi na upatikanaji wa chakula chao kwa urahisi, ndivyo polepole wanavyozidi kutapakaa sehemu tofauti za nchi ya Tanzania. Kwa mfano, mkoani Morogoro utaona kunguru mmoja mmoja katika manispaa ya morogoro, lakini baada ya miaka michache watakuwa wengi Sana. na inasadikika kuwa kutokana na kunguru kuweza kuishi kwenye hali ya hewa tofauti, basi katika miaka ijayo Mikoa yote ya Tanzania watapatikana.

No comments: